Kostanso wa Perugia

Mt. Kostanso na watakatifu wengine walivyochorwa na Perugino, 1497.

Kostanso wa Perugia (alifariki Foligno, Umbria, Italia, karne ya 3 hivi) alikuwa askofu wa kwanza wa mji huo akajitahidi kuinjilisha na kusaidia maskini.

Tangu zamani anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 29 Januari[1].

  1. Martyrologium Romanum

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search